Orodha ya majina ya walitwa kwenye Usaili Jeshi la Polisi Tanzania 2025

Image
  Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili – Jeshi la Polisi Tanzania 2025 Jeshi la Polisi Tanzania linapenda kuwataarifu waombaji wote waliotuma maombi ya kujiunga na jeshi hilo kwa mwaka 2025 kuwa mchakato wa usaili umeanza. Waombaji waliochaguliwa kwa ajili ya usaili wanatakiwa kufika kwenye vituo vya usaili wakiwa na nyaraka zifuatazo: Barua ya mwaliko wa usaili Nakala halisi na nakala ya cheti cha kuzaliwa Nakala halisi na nakala ya vyeti vya elimu (kidato cha nne/sita, astashahada, stashahada au shahada) Kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho kutoka NIDA Vyeti vya taaluma kwa waombaji wa fani maalum Picha mbili (2) za pasipoti za hivi karibuni Maelekezo Muhimu: Waombaji wote wanatakiwa kufika siku moja kabla ya tarehe ya usaili kwa ajili ya kuhakiki nyaraka zao Gharama za usafiri, malazi na chakula zitagharamiwa na mwombaji mwenyewe Usaili ni bure – hakuna malipo yoyote yanayohitajika Ni ...

TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA ZA JESHI LA POLISI TANZANIA - 2025

 

TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA ZA JESHI LA POLISI TANZANIA - 2025

Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza nafasi za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye sifa zinazotakiwa.

Sifa za Muombaji

  • Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa, pamoja na wazazi wake.
  • Awe amehitimu Kidato cha Nne au Sita kati ya mwaka 2019 hadi 2024.
  • Wenye elimu ya Astashahada, Stashahada au Shahada wawe na umri wa miaka 18-30.
  • Kidato cha Nne wawe na ufaulu wa Division I-IV (kwa Division IV, wawe na alama 26-28).
  • Kidato cha Sita wawe na ufaulu wa Division I-III.
  • Awe na urefu wa angalau 5’8” (wanaume) na 5’4” (wanawake).
  • Awe na kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya utambulisho.
  • Awe na afya njema kimwili na kiakili, hajaoa/kuolewa, na hana alama za kuchora mwilini (tattoo).
  • Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya Polisi na kufanya kazi mahali popote Tanzania.
  • Asiwe na historia ya uhalifu wala matumizi ya dawa za kulevya.

Utaratibu wa Kutuma Maombi

  1. Barua ya maombi iandikwe kwa mkono na iambatishwe kwenye mfumo wa PDF.
  2. Maombi yafanywe kupitia tovuti rasmi ya Jeshi la Polisi: https://ajira.tpf.go.tz
  3. Maombi yote yawasilishwe kabla ya tarehe 4 Aprili 2025.

Fani Zinazohitajika

  • Uhandisi (Civil, Electrical, Mechanical, Marine, Computer, etc.)
  • Sayansi ya Afya (Medical Doctor, Nursing, Pharmacy, Physiotherapy, etc.)
  • Teknolojia ya Habari (Cyber Security, Software Engineering, ICT, etc.)
  • Lugha na Mawasiliano (Journalism, Translation, Sign Language, etc.)
  • Masuala ya Sheria na Usimamizi (Law, Tax Management, Real Estate, etc.)

Kwa orodha kamili ya fani zinazotakiwa, angalia tangazo rasmi.

Maombi yote yasiyofuata utaratibu hayatazingatiwa!

Kwa maelezo zaidi, tembelea tovuti ya Jeshi la Polisi Tanzania.

TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA ZA JESHI LA POLISI TANZANIA - 2025


Bofya hapa kuanza Application

Trending Posts