Orodha ya majina ya walitwa kwenye Usaili Jeshi la Polisi Tanzania 2025
Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili – Jeshi la Polisi Tanzania 2025
Jeshi la Polisi Tanzania linapenda kuwataarifu waombaji wote waliotuma maombi ya kujiunga na jeshi hilo kwa mwaka 2025 kuwa mchakato wa usaili umeanza.
Waombaji waliochaguliwa kwa ajili ya usaili wanatakiwa kufika kwenye vituo vya usaili wakiwa na nyaraka zifuatazo:
- Barua ya mwaliko wa usaili
- Nakala halisi na nakala ya cheti cha kuzaliwa
- Nakala halisi na nakala ya vyeti vya elimu (kidato cha nne/sita, astashahada, stashahada au shahada)
- Kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho kutoka NIDA
- Vyeti vya taaluma kwa waombaji wa fani maalum
- Picha mbili (2) za pasipoti za hivi karibuni
Maelekezo Muhimu:
- Waombaji wote wanatakiwa kufika siku moja kabla ya tarehe ya usaili kwa ajili ya kuhakiki nyaraka zao
- Gharama za usafiri, malazi na chakula zitagharamiwa na mwombaji mwenyewe
- Usaili ni bure – hakuna malipo yoyote yanayohitajika
- Ni marufuku kutoa au kuahidi kutoa rushwa ili kupata ajira
Ratiba ya Usaili:
Ratiba kamili ya usaili (majina ya waombaji, tarehe na vituo vya usaili) inapatikana kwenye:
Kwa maelezo zaidi:
Barua pepe: co.recruitment@tpf.go.tz
Simu: +255 739 535 352
Imetolewa na:
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania
Tarehe: 23 Aprili 2025
BOFYA HAPA PAKUA HAPA TANZANIA LA KUITWA KWENYE USAIJILI JESHI LA POLISI KWA MWAKA 2025 (9.92 Mb)
